Kununua gari
Nitapataje gari?
Andika gari unalotaka kwenye kisanduku cha kutafuta, kama unavyolisema: “Prado”, “IST Dodoma”, “Harrier chini ya 40M” au “diesel automatic”. Utaona kila gari linalolingana, na unaweza kupunguza kwa Vichujio zaidi.
Je, Sukuma Ndinga inauza magari?
Hapana. Magari ni ya wamiliki binafsi na madila, na unashughulika nao moja kwa moja. Hatumiliki, hatuhifadhi wala hatukagui magari yaliyotangazwa, na hatuchukui pesa yoyote kwa ajili yake.
Nitawasilianaje na muuzaji?
Kila gari lina kitufe cha Piga simu na kitufe cha WhatsApp. Chini ya “Muulize muuzaji” kuna maswali tayari, kama “Bado linapatikana?”, yanayofungua WhatsApp swali likiwa limeshaandikwa.
Naweza kutoa bei ya chini?
Ndiyo. Andika bei yako chini ya “Toa ofa” kwenye ukurasa wa gari. Inamfikia muuzaji WhatsApp, na anaweza kukubali, kukataa au kutoa ofa nyingine.
“Bei nzuri” inamaanisha nini?
Yakiwepo angalau magari manne yanayofanana Sukuma Ndinga (chapa moja, miaka inayokaribiana), tunalinganisha bei zao na kuonyesha kama hili lina bei nzuri, ya kawaida au ya juu. Ni mwongozo, si tathmini ya thamani.
Naweza kuhifadhi magari?
Ndiyo. Bonyeza moyo kwenye gari lolote ulihifadhi chini ya Magari uliyohifadhi kwenye akaunti yako. Muuzaji akishusha bei, tutakutumia barua pepe.
Naweza kujulishwa gari ninalotaka likitangazwa?
Ndiyo. Andika unachotafuta chini ya Arifa za magari kwenye ukurasa wa mwanzo, au chini ya matokeo yoyote ya utafutaji, na uweke barua pepe yako. Tutakuandikia dakika moja gari linalolingana likitangazwa. Kila barua pepe ina kiungo cha kusimamisha arifa.
Amethibitishwa inamaanisha nini?
Tumekagua kitambulisho na namba ya simu ya muuzaji, na kwa dila pia leseni ya biashara na TIN. Haimaanishi tumekagua gari: siku zote ona gari na nyaraka zake mwenyewe.
Nalipa lini na vipi?
Unamlipa muuzaji moja kwa moja, na baada tu ya kuliona gari, kuliendesha na kukagua nyaraka zake. Kamwe usitume malipo ya awali kwa gari ambalo hujaliona. Soma vidokezo vyetu vya usalama kabla ya kununua.
Kukodi gari
Nakodije gari?
Fungua gari, chagua siku zako kwenye kalenda, andika unapotaka kulichukua na ni kwa ajili ya nini, kisha tuma ombi kwa WhatsApp. Mmiliki anakujibu huko na kuthibitisha.
Bei ni ya siku moja?
Ndiyo. Bei kwenye kila gari la kukodi ni ya siku moja. Ukichagua siku zako unaona jumla ya safari nzima.
Nalipa lini kwa kukodi?
Unamlipa mmiliki unapolichukua gari. Kubalianeni bei, amana yoyote, mafuta na muda wa kurudisha kabla ya kwenda, na muombe ayaandike.
Naweza kukodi na dereva?
Wamiliki wengi wanakodisha magari yao ya kujiendesha mwenyewe au na dereva. Muulize mmiliki kwenye ombi lako kipi kinakufaa.
Kutangaza gari lako
Kutangaza gari kunagharimu kiasi gani?
Hakuna. Kutangaza gari la kuuza au la kukodi ni bure.
Ninahitaji nini?
Picha nzuri, kadi ya usajili kwa mwaka na taarifa za injini, bei yako, na namba ya simu yenye WhatsApp. Anza hapa.
Gari langu litaonekana baada ya muda gani?
Kabla gari lako la kwanza halijaonekana, tunakagua wewe ni nani: namba yako ya simu na kitambulisho, na kwa madila leseni ya biashara na TIN. Unavituma kwenye Akaunti yangu, Wasifu wa muuzaji. Baada ya hapo tunakagua kila gari jipya, kwa kawaida ndani ya siku moja ya kazi.
Gari langu linakaa Sukuma Ndinga kwa muda gani?
Siku 30. Kwenye Akaunti yangu, chini ya Gereji yangu, unaweza kuongeza muda, kushusha bei, kuliweka kama limeuzwa au kulibadilisha wakati wowote.
Mimi ni dila. Naweza kutangaza magari yangu yote?
Ndiyo. Tangaza magari mengi kadiri ulivyo nayo kutoka akaunti moja. Magari yako yanapata ukurasa wa showroom yao, na wanunuzi wanaifikia timu yako moja kwa moja kwa simu au WhatsApp.
Akaunti yako
Ninahitaji akaunti?
Ili kutangaza gari au kuhifadhi magari tu. Kuangalia magari, kuwapigia wauzaji, kutuma maombi ya kukodi na arifa za magari hakuhitaji akaunti.
Nimesahau nenosiri langu
Chagua Ingia juu ya ukurasa, kisha “Umesahau nenosiri?”. Tutakutumia kiungo cha kuweka jipya.
Nafungaje akaunti yangu?
Tutumie ujumbe kutoka barua pepe au namba ya simu iliyo kwenye akaunti yako na tutaifunga na kuondoa magari yako.